Home AFCON 2023 Tembo wamfukuchua tai na kutwaa kombe la AFCON kwa mara ya tatu

Tembo wamfukuchua tai na kutwaa kombe la AFCON kwa mara ya tatu

0

Wenyeji Ivory Coast maarufu kama The Elephants ndio mabingwa wa makala ya 34 ya kombe la AFCON, baada ya kutoka nyuma na kuwazabua Super Eagles kutoka Nigeria mabao 2-1.

Fainali hiyo iliyosakatwa ugani Alassane Ouattara mjini Abidjan Jumapili usiku ilishuhudiwa na zaidi  ya mashabiki 60,000.

Super Eagles walichukua uongozi mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupitia kwa nahodha Troost Ekong, kabla Frankie Kessie kusawazishia wenyeji dakika ya 62.

Sebastien Haller alipachika bao la ushindi la dakika ya 81 na kuwanyanyua mashabiki wa nyumbani.

Ilikuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006 kwa waandalizi kunyakua kombe hilo, Misri ikitawazwa mabingwa wakati huo.

Ivory Coast waliandaa kombe la AFCON  kwa mara ya kwanza mwaka 1992 na 2015 kwa mara ya pili.