Home AFCON 2023 Tembo wa Ivory Coast wapigwa radi nyumbani

Tembo wa Ivory Coast wapigwa radi nyumbani

0

Matumaini ya wenyeji Ivory Coast kufuzu kwa raundi ya 16 bora yamedidimia Jumatatu jioni baada, ya kuambulia kichapo cha mabao manne kwa bila kutoka kwa Equitorial Guinea katika mchuano wa mwisho wa kundi A uliosakatwa Jumatatu jioni.

Emilio Nsue alitikisa nyavu mara mbili kwa Equitorial Guinea maarufu kama National Lighting, huku Pablo Ganet na Jannick Buyla kuongeza moja kila mmoja, huku mashibi wa timu ya nyumbani wakiduwazwa .

Ivory Coast inanusia kubanduliwa mashindanoni ikiwa na pointi 3 pekee katika nafasi ya tatu huku Equitorioal Guinea wakiongoza kwa alama 7 wakifuatwa na Nigeria pia kwa pointi saba baada ya kuwabwaga Guinea Bissau bao moja kwa bila.

Website | + posts