Home Habari Kuu Tembo amng’ata Simba na kumvua ubingwa wa AFCON

Tembo amng’ata Simba na kumvua ubingwa wa AFCON

0
Ivory Coast's midfielder #8 Franck Kessie (C) celebrates after scoring his team's first goal from the penalty spot during the Africa Cup of Nations (CAN) 2024 round of 16 football match between Senegal and Ivory Coast at the Stade Charles Konan Banny in Yamoussoukro on January 29, 2024. (Photo by KENZO TRIBOUILLARD / AFP)

Wenyeji Ivory Coast walijizatiti kisabuni na kuwavua ubingwa Senegal baada ya kuwalemea kwa mabao 5-4 na kufuzu kwa robo fainali  kupitia matuta ya penalti baada ya timu zote kuambulia sare ya 1-1 katika dakika 120.

Habib Diallo aliwaweka Simba wa Teranga kifua mbele kunako dakika ya 4 ya  mechi hiyo ya awamu ya 16 bora, akiunganisha pasi ya Sadio Mane.

Tembo wa nyumbani walijituma na kuendelea kumiliki mpira kwa kipindi kirefu na mashambulizi tele yaliyozaa matunda baada ya kupata penalti ya 86 iliyofungwa na nahodha Frankie Kessie na kulazimisha muda wa mazidadi.

Katika hatua ya matuta, Ivory Coast waliunganisha mikwaju yote huku beki Moussa Niakhate akigonga chuma.

Ilikuwa mara ya saba mtawalia kwa mabingwa watetezi wa AFCON kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

 

Website | + posts