Home Kimataifa Tebogo amfyatua Lyles na kutawazwa bingwa wa Olimpiki wa mita 200

Tebogo amfyatua Lyles na kutawazwa bingwa wa Olimpiki wa mita 200

0
kra

Letsile Tebogo wa Botswana ndiye bingwa mpya wa Olimpiki wa mita 200 katika mashindano ya Paris, Ufaransa baada ya kumduwaza Noah Lyles wa Marekani.

Chipukizi huyo aliye na umri wa miaka 21 alizitimka mbio hizo kwa sekunde 19.46 Alhamisi usiku akiandikisha historia kuwa Mwafrika wa kwanza kutwaa dhahabu ya Olimpiki katika shindano hilo.

kra

Keneth Bednarek wa Marekani alinyakua nishani ya fedha kwa sekunde 19.62 huku bingwa wa Dunia Lyles pia akihifadhi shaba aliyoishinda katika Olimpiki iliyopita kwa sekunde 19.70.

Website | + posts