Home Kimataifa Novemba 13 yatangazwa sikukuu ya kupanda miti

Novemba 13 yatangazwa sikukuu ya kupanda miti

0

Serikali imetangaza kuwa tarehe 13 mwezi huu itakuwa siku kuu ya upanzi wa miti kote nchini wakati huu wa msimu wa mvua.

Tangazo hilo lilitolewa jana Jumatatu jioni kupitia gazeti rasmi la serikali na kutiwa saini na Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki.

Wakati wa likizo hiyo, wananchi kote nchini watahitajika kupanda miti kama mchango wao kwa juhudi za kitaifa za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi nchini.

Kindiki hata hivyo alisema mitihani ya kitaifa itaendelea kama ilivyopangwa.

Waziri alidokeza kuwa maeneo maalum ya kitaifa yatatengwa kwa ajili ya shughuli hiyo ya upanzi wa miti, itakayoongozwa na Rais William Ruto na kuhudhuriwa na mawaziri wote.

Shughuli hiyo ni ishara ya kujitolea kwa taifa hili kuhifadhi mazingira na kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi kote duniani.

Website | + posts