Home Burudani Tanzia: Mwanamuziki wa pwani Ali B amefariki

Tanzia: Mwanamuziki wa pwani Ali B amefariki

0

Mwanamuziki wa eneo la Pwani Ali B amefariki.

Inadaiwa kwamba mwimbaji huyo amekuwa akiugua kile kinachodhaniwa kuwa ugonjwa wa Nimonia na alifariki katika hospitali ya Makadara mjini Mombasa.

Mwili wake huenda utazikwa kesho Ijumaa, kulingana na mipangilio ya dini ya kiisilamu.

Watu wengi wamemwomboleza Ali B mitandaoni akiwemo mwanasiasa na mwanabiashara wa Mombasa Suleiman Shahbal.

Shahbal alisema ameshtushwa na taarifa za kifo cha mwimbaji huyo aliyemrejelea kuwa rafiki ambaye alikuwa karibu naye muda wote kwenye siasa.

Ameitakia familia ya mwimbaji huyo faraja wakati huu wa maombolezi.

Aliyekuwa mtangazaji wa Radio Taifa Mwinyi Kazungu ameandika, “Ninaweza kuongea mengi kukuhusu. Niseme mazuri kwa mchango wako mkubwa kwenye tasnia ya muziki pwani yetu na yote sitayamaliza. Ushamaliza safari yako duniani ndugu yangu. Mie nikusema tu Innallillah Wainna illaihi Rajuin Ali B.”

Tutakufahamisha mengi kadri tutakoyapokea kuhusu taarifa hii.

Website | + posts