Home Habari Kuu Tanzania kujenga kituo cha uwekezaji na afisi za ubalozi Nairobi

Tanzania kujenga kituo cha uwekezaji na afisi za ubalozi Nairobi

0
kra

Waziri aliye na Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje jana Jumanne aliongoza hafla ya kuipa Tanzania ardhi ya kujenga kituo cha uwekezaji na afisi za ubalozi jijini Nairobi.

Mudavadi alimpokeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba kipande hicho cha ardhi katika eneo la Upper Hill.

kra

Alisema hatua hiyo inaashiria wakati muhimu katika uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili na inaimarisha uhusiano huo mbali na kudhihirisha kujitolea kwa Kenya kuendeleza ushirikiano.

Tanzania itajenga majengo mawili yenye orofa 22 kila moja katika kipande hicho cha ardhi ambayo yatatumiwa kukuza ushirikiano wa kiuchumi, ubunifu na ufanisi wa pamoja.

Kwa upande wake, Makamba alisisitiza kwamba mradi huo ni sehemu ya awamu ya sita ya mkakati wa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan unaolenga kutumia ipasavyo ardhi za nchi hiyo ng’ambo ili kuongeza mapato ya taifa.

Mawaziri Peninah Malonza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rebecca Miano wa Biashara walihudhuria hafla hiyo wakiwa na mabalozi kadhaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here