Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia, kama njia ya kuimarisha usalama wa nishati na ukuzaji uchumi kwa mataifa yote mawili.
Bomba hilo litasafirisha gesi asilia kutoka Kusini mwa Tanzania hadi Uganda ambapo itatumika viwandani na kuzalisha umeme.
Mkataba huo ulisainiwa kati ya Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Doto Biteko na Waziri wa Uganda wa Nishati na Maendeleo ya Madini Ruth Nankabirwa.