Home Burudani Tamasha la Walker Town: Kampuni ya EABL kuwarejeshea mashabiki fedha

Tamasha la Walker Town: Kampuni ya EABL kuwarejeshea mashabiki fedha

0
kra

Kampuni ya mvinyo ya East African Breweries (EABL), imeomba msamaha kufuatia changamoto zilizoshuhudiwa na mashabiki, washirika na wasanii wakati wa tamasha la Walker Town, Jijini Nairobi.

“Tunaomba msamaha kwa kila mmoja aliyeathiriwa na tamasha hilo,” ilisema taarifa ya kampuni ya EABL.

kra

Huku ikiahidi kurejesha fedha kwa mashabiki waliohudhuria tamasha hiyo siku ya pili, kampuni hiyo iliomba msamaha baada ya msanii maarufu wa Marekani Lauryn Hill kuchelewa kutumbuza, huku msanii wa hapa nchini Nyashinski, akikosa kuwatumbuiza mashabiki.

“Licha ya juhudi zetu za mchwa, tulikumbwa na changamoto ambazo hatungeweza kuziepuka, hasaa mvua na maswala mengine yaliathiri mitambo ya sauti,” ilisema kampuni hiyo.

Tamasha la WalkerTown, lililoandaliwa katika bustani ya Laureate, Kasarani mwishoni mwa wiki, liligonga vichwa vya habari kutokana na wasanii wa hadhi ya juu waliokuwa wamealikwa.

Mashabiki waliohudhuria siku ya Jumapili, waliondoka katika bustani hiyo Jumatatu asubuhi baada ya kusubiri kwa saa kadha Lauryn Hill kuwatumbuiza.

Website | + posts