Home Burudani Tamasha ya Kileleshwa

Tamasha ya Kileleshwa

0

Wakazi wa wadi ya Kileleshwa kaunti ya Nairobi, kupitia kwa shirikisho lao linalofahamika kama KIWANA wamepanga tamasha ya kwanza kabisa kwa jina “KileFest” kwa lengo la kukuza umoja na kusherehekea utofauti wao.

Kulingana na waandalizi wa tamasha hiyo, dhamira nyingine ni kuhakikisha wanajali majirani hasa wasiobahatika na ambao wanahitaji usaidizi.

Tamasha hiyo ambayo itaandaliwa Agosti 19, 2023 ilizinduliwa mnamo Julai 6, 2023 katika kikao ambacho kilihudhuriwa na Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja na mwakilishi wa wadi ya Kileleshwa Robert Alai.

Gavana Sakaja alisema kwamba mashirikisho ya jamii kama vile KIWANA ni nguzo muhimu katika ushirikiano kati ya viongozi na wananchi.

Siku hiyo kutakuwa na michezo kama vile soka na mingine ya watoto na watu wazima.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here