Home AFCON 2023 Takwimu za kindumbwendumbwe cha AFCON nchini Ivory Coasu

Takwimu za kindumbwendumbwe cha AFCON nchini Ivory Coasu

0

Makala ya 34 ya kindumbwendumbwe cha kuwania kombe la mataifa ya Afrika AFCON yataingia awamu ya 16 bora baina ya Jumamosi  Januari 27 na Jumanne Januari 30 nchini Ivory Coast.

Mataifa 16 yaliyosalia mashindano ni:Wenyeji Ivory Coast,Nigeria,Equitorial Guinea,Misri,Cape Verde,Angola,Namibia,Mauritania,Cameroon,Senegal,Morocco,Afrika Kusini,,DR Congo,Guinea ,Burkina Faso na Mali .

Timu zilizoyaaga mashindano katika hatua ya makundi ni ;-Algeria,Ghana,Guinea Bissau,Msumbiji,Tunisia,Zambia na Tanzania .

Mechi 36 zimechezwa kufukia sasa na mabao 89 kufungwa.

Emmilio Nzue wa Equitorialk Guinea ndiye mfungaji bora akiwa na mabao 5 akifuatwa na  Baghdad Bounedjah wa Algeria na Mostafa Mohamed wa Misri kwa magoli matatu kila mmoja.

Waandinga wanane wafunga magoli mawili kila mmoja wakiwa:-Gelson Dala na Mabululu wote kutoka Angola,Bertrand Traore wa Burkin Faso,Jordan Ayew na Mohammed Kudus wote kutoka Ghana, Lassine Sinayoko wa Mali,Lamine Camara wa Senrgal na Themba Zwane wa Afrika Kusini.

Magoli ya kujifunga katika kipute hicho ni ya:Esteban Orozco wa Equatorial Guinea wakicheza na Guinea-Bissau,James Gomez wa Gambia wakicheza dhidi ya Cameroon na Opa Sanganté wa Guinea-Bissau wakichuana na Nigeria.

Wanandinga waliopigwa kadi nyekundu ni ;Eboue Adams wa Gambia,Francois Kamano wa Guinea,Novatus Miroshi wa Tanzania na Roridrick Kabwe wa Zambia.