Home Michezo EURO 2024: Takwimu muhimu za Ufaransa dhidi ya Poland

EURO 2024: Takwimu muhimu za Ufaransa dhidi ya Poland

Katika historia yao ya pamoja, Ufaransa na Poland wamekutana mara 17 uwanjani.

0
Mshambuliaji wa Ufaransa #10 Kylian Mbappe (kushoto) akipambania mpira na Kiungo wa Poland #20 Piotr Zielinski wakati wa michuano ya kombe la dunia huko Qatar kwenye raundi ya 16 ya michuano kati ya Ufaransa na Poland kwenye Dimba la Al-Thumama jijini Doha, Disemba 4, 2022. (Picha kwa hisani ya FRANCK FIFE / AFP)
kra

Juni 25, 2024, uwanja wa nyumbani wa klabu ya Borussia Dortmund kaskazini mwa Rhine-Westphalia nchini Ujerumani kutawaka moto wakati Ufaransa na Poland zitakapomenyana kwenye mechi za kuwania ubingwa wa bara ulaya. Kwa Poland, mchuano huo utakuwa ni mchezo wa majivuno kwani ilivyo kwa sasa, watakuwa wanaelekea nyumbani hata wakiushinda. 

Ufaransa itamenyana na Poland huko Dortmund ikiwa na nia ya kumaliza michuano ya mechi za makundi kwa kuongoza kundi lao la D kuelekea droo ya hatua ya muondoano wa michuano ya Euro 2024.

kra

Nafasi ya Ufaransa katika hatua ya 16 bora ilipatikana kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Uholanzi, lakini bado wanahitaji kuimarika ikiwa wanataka kutoka kibabe kundi D.

Lakini ikiwa Uholanzi itashinda mechi yao dhidi ya Austria, na Ufaransa ishindwe kupata ushindi, Uholanzi itachukua nafasi ya kwanza kwenye kundi hilo kutokana na tofauti ya mabao.

Lewandowski (Kulia) akipambania mpira dhidi ya beki wa Austria kwenye mashindano ya Euro 2024

Timu ya Taifa ya Poland imeshindwa kujichomoa kwenye kundi hilo kufuatia matokeo mabovu kwenye mechi zao mbili walizotangulia kucheza, hivyo basi mchezo wa kesho Jumanne utakuwa wa kufurahisha nyoyo zao tu kisha warejee makwao.

Katika historia yao ya pamoja, Ufaransa na Poland wamekutana mara 17. Kwenye mashindano hayo 17, Ufaransa imeshinda mara tisa (9), Poland wakishinda mara tatu (3) huku michezo mitano ikiisha sare.

Katika mechi yao ya mwisho ya timu hizi mbili kukutana ilikuwa ni kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2022, ambapo Ufaransa iliicharaza Poland magoli 3-1.

SOMA ZAIDI: Uswizi na Ujerumani zafuzu awamu ya pili ya Euro

Ufaransa vs Poland: Mechi tano za mwisho

  • 04 Dec 2022: France 3-1 Poland (Kombe la Dunia)
  • 09 Jun 2011: Poland 0-1 France (mechi ya kirafiki)
  • 17 Nov 2004: France 0-0 Poland (mechi ya kirafiki)
  • 23 Feb 2000: France 1-0 Poland (mechi ya kirafiki)
  • 16 Aug 1995: France 1-1 Poland (mechi ya EURO)

Jumla ya mechi na matokeo ya ushindi: Ufaransa vs Poland 

  1. Mechi: 17
  2. Ufaransa – 9
  3. Poland – 3
  4. Sare – 5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here