Home Habari Kuu Kenya kupokea kiwango kikubwa cha mvua za vuli

Kenya kupokea kiwango kikubwa cha mvua za vuli

Mvua hiyo kubwa inayotarajiwa inatokana na joto jingi katika bahari ya Pacific ya Kati na Mashariki ya ikweta ikiashiria uwepo wa hali ya El Nino.

Kenya kupokea kiwango kikubwa cha mvua. Picha/ Hisani.

Nchi hii inatarajiwa kupata kiasi kikubwa cha mvua wakati wa msimu wa mvua za vuli, kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba.

Mkurugenzi wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa Dkt. David Gikungu amesema msimu huo utakuwa muhimu kwa nchi hii hasa kwa maeneo ya kati na mashariki.

Dkt. Gikungu alisema huenda baadhi ya maeneo yakapokea mvua kubwa ya hadi milimita 700 hususan katika maeneo ya nyanda za juu za eneo la katikati mwa nchi.

Aidha, alisema kuwa mvua itanyesha kwa usawa katika maeneo mengi. Idara hiyo ilisema kuwa kaunti za eneo la Kaskazini Mashariki ambazo zimeshuhudia kipindi kirefu cha kiangazi, zinatarajiwa kupata mvua nyingi.

Dkt. Gikungu alisema mvua hiyo kubwa inayotarajiwa inatokana na joto jingi katika bahari ya Pasific ya Kati na Mashariki ya ikweta ikiashiria uwepo wa hali ya El Nino.

Alitoa wito kwa sekta kama vile kilimo, maji na kawi kutumia mvua hiyo kuongeza uzalishaji chakula.

Website | + posts
Judith Akolo
+ posts