Home AFCON 2023 Tai wa Nigeria watinga fainali ya AFCON kwa taabu

Tai wa Nigeria watinga fainali ya AFCON kwa taabu

0
kra

Licha ya kupitia changamoto tele katika dakika 120, Super Eagles ya Nigeria hatimaye walitinga fainali ya kombe la AFCON baada ya subira ya miaka 11.

Nigeria walizidiwa kimchezo na Bafana Bafana ya Afrika Kusini katika nusu fainali ya kwanza iliyopigwa Jumatano usiku katika uwanja wa Bouke, huku wakilazimishwa kutoka sare ya bao moja ndani ya dakika 90.

kra

Nahodha Troost Ekong aliwaweka Nigeria uongozini katika dakika ya 65 kupitia penalti, kabla ya Teboho Mokoena kuisawazishia Bafana kunako dakika ya 90.

Timu zote zilitoka sare tena katika dakika 30 za mazidadi na kulazimu mshindi abainike kupitia changamoto ya matuta ya penalti.

Nigeria walifunga penalti nne na kupoteza moja huku Afrika Kusini wakifunga penalti mbili pekee.

Super Eagles watarejea mjini Abidjan Jumapili, Februari 11 wakiwania kombe la nne na la kwanza tangu mwaka wa 2013.