Home AFCON 2023 Tai wa Nigeria wakanyaga tembo wa Ivory Coast

Tai wa Nigeria wakanyaga tembo wa Ivory Coast

0

Super Eagles ya Nigeria iliwanyima wenyeji Ivory Coast raha baada ya kuizabua goli moja kwa bila katika mechi ya kundi A iliyopigwa jana Alhamisi usiku.

Bao pekee la ushindi la tai wa Nigeria lilipachikwa kimiani na nahodha Troost Ekong kupitia penalti, baada ya Victor Osimhen kuchezewa ngware mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Mchuano huo haukuwa na msisimko timu zote zikibuni nafasi haba za kufunga magoli.

Equatorial Guinea wanaongoza kundi A kwa pointi 4 sawa na Nigeria iliyo ya pili, huku The Elephants ikiwa na pointi 3 katika nafasi ya tatu.

Ivory Coast ni sharti washinde mchuano wa mwisho dhidi ya Equatorial Guinea Jumatatu ijayo ili kufuzu moja kwa moja kwa raundi ya 16 bora.

Website | + posts