Home AFCON 2023 Tai wa Mali wapaa hadi robi fainali AFCON

Tai wa Mali wapaa hadi robi fainali AFCON

0

Mali walijikatia tiketi kwa robo fainali ya kombe la AFCON baada ya kuwalaza Burkina Faso mabao 2-1, katika mchuano wa raundi ya 16 bora uliosakatwa Jumanne usiku katika uga wa Amodou Gon Coulibally nchini Ivory Coast.

Edmond Tapsoba alijifunga na kuwaweka Eagles uongozini mwanzoni mwa kipindi cha kwanza huku Lacine Sinayoko, akitanua uongozi mwanzoni mwa kipindi cha pili kabla ya Betrant Traore kukomboa moja kupitia penati.

Mali watamenyana na wenyeji Ivory Coast katika robo fainali.

Website | + posts