Ziara ya siku 4 ya Mfalme Charles imeanza rasmi leo, siku moja tu baada ya kuwasili humu Nchini akiambatana na mkewe malkia Camilla chini ya ulinzi mkali.
Hii ni mara ya Nne kwa Mfalme Charles wa Tatu kutembelea Kenya. Wafalme wengine kutembelea Kenya pia ni pamoja na Malkia Elizabeth wa 2, mkuu wa Wales, Duke na Duchess wa Edinburg, Princess Royal, Duke na Duchess wa Gloucester na Princess Alexandra. AUSTIN MIRAMBO alikuwa katika ikulu ya rais na kutuandalia ripoti ifuatayo.