Home Michezo Uswidi yafuzu nusu fainali ya 5 ya Kombe la Dunia

Uswidi yafuzu nusu fainali ya 5 ya Kombe la Dunia

0
AUCKLAND, NEW ZEALAND - AUGUST 11: Filippa Angeldal (3rd R) of Sweden celebrates with teammates after scoring her team's second goal during the FIFA Women's World Cup Australia & New Zealand 2023 Quarter Final match between Japan and Sweden at Eden Park on August 11, 2023 in Auckland, New Zealand. (Photo by Buda Mendes/Getty Images)
kra

Uswidi imefuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya 5 baada ya kuwabwaga Japani mabao 2-1 katika robo fainali iliyopigwa ugani Eden Park mjini Auckland, New Zealand leo Ijumaa.

Amanda Ilestedt na Filippa Angeldal walipachika bao moja kila mmoja katika kila nusu ya mchezo huku Japani wakipata bao la pekee kupitia kwa Honika Uashi dakika tatu kabla ta kipenga cha mwisho.

kra

Uswidi watapambana na Uhispania katika nusu fainali ya kwanza.

Robo fainali mbili za mwisho za Kombe la Dunia zitachezwa kesho Jumamosi huku Ufaransa ikimenyana wenyeji Australia kuanzia saa nne asubuhi kabla ya mabingwa wa Ulaya kumaliza udhia dhidi ya wakuza kahawa Colombia kuanzia saa saba unusu adhuhuri.

Website | + posts