Home Burudani Suzanna Owiyo afiwa na mamake

Suzanna Owiyo afiwa na mamake

0

Mwanamuziki Suzanna Owiyo ametangaza kwamba mamake mzazi ameaga dunia. Kupitia mtandao wa X ambao awali ulijulikana kama Twitter, Owiyo alisema haamini kwamba hilo limetokea.

Alimsherehekea mamake akisema amekuwa nguzo muhimu katika maisha yake na ambaye ujasiri wake ulirahisisha maisha.

“Asante mama kwa kila kitu ambacho umefanya. Ulisimama kama nguzo muhimu kwa familia na kufanya changamoto za maisha ziwe rahisi.” aliandika Suzanna.

Aliongeza kusema kwamba ukarimu, ujasiri, uhalisia na uaminifu wake viliacha alama kwa maisha yao.

Kifo cha mama Suzanna kinajiri miaka mitatu baada ya kifo cha babake ambaye wakati huo alimtaja kuwa mfano mzuri kwa maisha yake.

Mwezi Januari mwaka huu alifanya ukumbusho wa babake.

Mashabiki wake wengi wamemwandikia jumbe za kumfariji wakati huu ambapo anaomboleza.

Owiyo ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo ambaye pia ni mtetezi. Mwaka 2011, alishinda tuzo ya rais iitwayo “Grand Warrior of Kenya” kutokana na mafanikio yake kwenye tasnia ya muziki ndani na nje ya Kenya.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here