Home Kimataifa Sudan Kusini yajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa kwanza tangu mwaka 2011

Sudan Kusini yajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa kwanza tangu mwaka 2011

0

Sudan Kusini imeanza mchakato wa uchaguzi mkuu huku waangalizi wa kimataifa wakihofia uwezo wa taifa hilo kuandaa uchaguzi huru na wa haki kutokana na ukosefu wa usalama.

Kama njia mojawapo ya maandalizi Sudan Kusini imeanza usajili wa wapiga kura kote nchini humo .

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya Uchaguzi NEC,Abednego Akok Kacuol,wamewatuma maafisa wa uchaguzi katika majimbo yote kumi na wako tayari kwa uchaguzi.

Sudan Kusini haijafanya uchaguzi mkuu tangu Rais Salva Kiir achaguliwe mwaka 2011.

Taifa hilo lilipanga kuandaa uchaguzi wa kwanza Februari mwaka uliopita baada ya kumalizika kwa vita mwaka 2018

Website | + posts