Home Taifa SRC yatupilia mbali nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa serikali

SRC yatupilia mbali nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa serikali

0
kra

Tume ya Mishahara na Marupurupu SRC imesimamisha mpango wake wa kuwapa maafisa wa serikali nyongeza ya mishahara.

Akihutubia wanahabari Jumatano, Mwenyekiti wa SRC Lyn Mengich alifichua kwamba tume hiyo ilisimamisha nyongeza hayo baada ya mashauriano na Hazina ya Kitaifa. Mengich pia alihusisha hatua hiyo na matatizo ya kiuchumi baada ya kupunguzwa kwa bajeti ya mwaka wa 2024/2025.

kra

Hata hivyo, mwenyekiti huyo wa SRC alitetea uamuzi wa awali wa tume hiyo kuongeza mishahara, akisema kuwa ni kwa mujibu wa sheria. Kulingana na Bi Mengich, tume hiyo ina jukumu la kukagua mishahara ya wafanyikazi wote wa umma baada ya miaka miwili, na notisi ya kuongeza malipo ya wabunge ilitangazwa kwenye gazeti la serikali Agosti mwaka jana. Aliongeza kuwa tume hiyo ilikosa kukagua mishahara kwa miaka miwili kufuatia madhara yaliyoletwa na janga la COVID-19 mnamo 2020.

Matamshi ya SRC yanafuatia pingamizi kali miongoni mwa umma , baada ya ripoti kuwa tume hiyo ilikusudia kuongeza mishahara kwa maafisa wa Serikali wakati ambapo maandamano kutokana na matatizo ya kiuchumi yanaendelea humu nchini.

Baadhi ya wabunge na maseneta walijitokeza kukashifu tume hiyo huku wengine wakishinikiza kuvunjwa kwa SRC, kwa kutojali masuala yanayoathiri nchi. Rais William Ruto pia alijitokeza kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapendekezo hayo ya kuongeza mishahara.

Jemie Saburi
+ posts