Home Kimataifa Spika Wetangula asema rungu ya bunge haikuibwa

Spika Wetangula asema rungu ya bunge haikuibwa

0
Spika wa Bunge la taifa Moses Wetangula.

Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula amebainisha kwamba rungu ya bunge haikuibwa wakati waandamanji waliingia katika majengo ya bunge jana.

Akihutubia bunge leo asubuhi, Wetangula alikanusha ripoti za kuibwa kwa rungu hiyo akisema kwamba kilichoibwa ni mwigo wa rungu hiyo ambayo ni muhimu katika kuendesha shughuli za bunge.

Mwigo huo kulingana naye huwa umewekwa mahali ambapo unaonekana na wote wanaofika katika bunge la taifa.

Wetangula alihakikishia wabunge kwamba rungu hiyo iko chini ya ulinzi mkali huku akisisitiza umuhimu wa kifaa hicho bungeni.

Rungu hiyo au “Mace” katika lugha ya kiingereza ni mojawapo ya vifaa muhimu vya bunge na huwa inaashiria mamlaka ya bunge na ni lazima iwe mezani katikati ya bunge ili kuhalalisha yanayotekelezwa bungeni.

Katika mabunge mengi ulimwenguni, hakuna mipango inaweza kuendelea humo iwapo rungu hiyo haipo na katika utawala wa kifalme, rungu hiyo hutumiwa kuashiria mamlaka ya kifalme.

Website | + posts