Home Habari Kuu Spika Wetang’ula aidhinisha hoja ya kumtimua waziri Mithika Linturi

Spika Wetang’ula aidhinisha hoja ya kumtimua waziri Mithika Linturi

Wamboka sasa anataka kubuniwa kwa kamati maalum kuchunguza madai yaliyotolewa dhidi yake.

0
Waziri wa kilimo Mithika Linturi.

Hatma ya waziri wa kilimo Mithika Linturi, sasa imo mikononi mwa wabunge wa taifa baada ya spika Moses Wetang’ula, kuidhinisha hoja ya kumuondoa mamlakani.

Hoja ya kumtimua waziri huyo iliwasilishwa katika bunge la taifa na mbunge wa Bumula Jack Wamboka, huku akimshtumu waziri huyo kwa kutoa habari ambazo hazikuwa sahihi kwa kamati za bunge kuhusu uuzaji wa mbolea bandia za bei nafuu.

Katika mawasiliano yake kwa kikao cha leo Jumanne cha bunge, Wetangula alisema hoja iliyowasilishwa na mbunge wa Bumula, Jack Wamboka, imetimiza mahitaji ya kujadiliwa bungeni.

Wamboka sasa anataka kubuniwa kwa kamati maalum kuchunguza madai yaliyotolewa dhidi yake.

Katika hoja yake, Wamboka anamshtumu Linturi kwa kukiuka  katiba, utovu wa nidhamu na kuwasilisha taarifa za kupotosha kwa kamati za bunge zilizokuwa zikichunguza sakata ya uuzaji wa mbolea bandia kwa wakulima.

Hoja hiyo ya kumuondoa mamlakani waziri Linturi, iliungwa mkono na mbunge wa Laikipia kaskazini Sarah Korere.

Website | + posts