Home Habari Kuu Spika Wetang’ula apiga marufuku suti za ‘kaunda’ bungeni

Spika Wetang’ula apiga marufuku suti za ‘kaunda’ bungeni

0

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula amepiga marufuku mavazi yasiyo rasmi bungeni zikiwemo suti za “kaunda” wakati wa vikao.

Wetang’ula alisitiza haja ya wabunge kuzingatia kanuni zilizopo za mavazi wanapohudhuria vikao ikiwa ni suruali refu, shati la mikono mirefu, tai, soksi pamoja na koti huku wabunge wanawake wakihitajika kuvalia gauni refu au sketi inayopita magoti na wasivalie blausi za mikono mifupi.

Website | + posts