Home Michezo Song ataja kikosi cha Cameroon kwa kipute cha AFCON

Song ataja kikosi cha Cameroon kwa kipute cha AFCON

0

Kocha wa Cameroon Rogobert Song, ametaja kikosi cha awali cha wanandinga 27 watakaoshiriki makala ay 34 ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 mwaka ujao.

Cameroon maarufu kama Indomitable Lions itakuwa ikishiriki AFCON kwa mara ya 21 wakijivunia kutawazwa mabingwa mara tano.

Vijana wa Song walionyakua kombe hilo kwa mara ya mwisho mwaka 2017 wamejumuishwa kundi C pamoja na Teranga Lions ya Senegal ambao ni mabingwa watetezi, Gambia na Guinea.

Kikosi kilichotajwa kinawajumuisha André Onana kiungo André-Frank Zambo Anguissa na washambulizi Karl Toko-Ekambi,Vincent Aboubakar na Clinton Njié.

Kikosi cha mwisho cha wachezaji 24 kinatarajiwa kutangazwa kabla ya Januari 3 ambayo ni siku ya makataa iliyowekwa na CAF.