Home Kimataifa Somaliland yakataa kuunganishwa na Somalia

Somaliland yakataa kuunganishwa na Somalia

0

Taifa la Somaliland likemektaa kata kata mazungumzo yoyote yanayopendekeza kuunganishwa na Somalia.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Somaliland, imesema iko tayari kwa majadiliano yoyote yatakayosaidia taifa hilo kusonga mbele kama nchi huru wala sio kuunganishwa na Somalia.

Taarifa hii inajiri siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kujitolea kuongoza mazungumzo ya kuunganishwa kwa mataifa hayo mawili alipokutakana na mjumbe maalum wa Somaliland Muse Jama katika Ikulu ya Uganda.

Somaliland ilijitenga kutoka Somalia mwaka 1991 lakini uhuru wake haujatambulika kimataifa.