Home Habari Kuu Somalia yamtuma bi Fazia kumpinga Raila kwa uenyekiti wa AU

Somalia yamtuma bi Fazia kumpinga Raila kwa uenyekiti wa AU

0

Somalia imeanza kampeini za kumpigia debe aliyekuwa waziri Fawzia Adam kuwania uenyekiti wa Muungano wa Afrika,AU kupambana na Raila Odinga aliyependekezwa na serikali ya Kenya.

Fununu zilianza kuzagaa tangu mwezi Januari mwaka huu, kuhusu uwezekano wa Bi Fawzia aliyekuwa waziri wa kigeni wa kwanza wa kike nchini Somalia kuwania kiti hicho.

Ujio wake unatoa changamoto ya moja kwa moja kwa Odinga, na kutia dukuku uwezekano wa Somalia kuunga mkono Kenya katika harakati hizo.

Kulingana na maafikiano ya mwaka 2018 Afrika Mashariki itakuwa na zamu ya kumtoa mwenyekiti wa kamati ya AU, katika uchaguzi wa Februari mwaka ujao  ingawa EAC iko huru kuwasilisha wagombeaji wengi itakavyo.

Website | + posts