Home Kaunti Soko la Kibuye lateketea

Soko la Kibuye lateketea

0

Wafanyabiashara wanakadiria hasara katika soko la Kibuye iliyoko kaunti ya Kisumu baada ya moto kuteketeza vibanda vyao leo Jumatatu asubuhi.

Benjamin Oyugi ambaye ni mlinzi katika soko hilo alielezea yaliyotokea na kusema kuwa chanzo cha moto huo hakijabainika.

“Niliitwa wakati moto ulipolipuka. Mara moja tulianza kuchukua hatua, lakini kufikia wakati huo, moto ulikuwa tayari umeteketeza maduka na hoteli ndogo,” Oyugi alieleza.

Hakuna maafa yaliyotokea katika kisa hicho wala majeruhi kuripotiwa.

Mmoja wa wafanyabiashara Mary Goreti Atieno ambaye kibanda chake kilichomeka alielezea masikitiko yake baada ya mkasa huo.

“Nilifanikiwa kuokoa beti langu la nguo kabla ya kuteketezwa na moto. Inasikitisha kuona uharibifu, lakini ninashukuru kwamba hakuna maisha yaliyopotea,” alisema Atieno.

Mwenyekiti wa soko hilo Judith Odhiambo alisikitikia uharibifu wa mali na kuwaomba wafanyabiashara kuwa waangalifu ili kuepukana na visa kama hivyo.

“Ni bahati mbaya sana kwamba moto uliharibu soko letu na kuharibu bidhaa muhimu. Hata hivyo, hii inatumika kama ukumbusho kwa kila mtu kuwa waangalifu zaidi katika kulinda mali zao,” alisema.

Maafisa wa usalama wameanzisha uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.