Home Habari Kuu Sita waangamia kwa virusi vya Marburg nchini Rwanda

Sita waangamia kwa virusi vya Marburg nchini Rwanda

0
kra

Watu sita wamethibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Marburg nchini Rwanda huku wengine 20, wakiripotiwa kuambukizwa kulingana na wizara ya afya nchini humo.

Waziri wa afya nchini Rwanda Sabin Nsanzimana ametangaza hayo jana huku akiongeza kuwa wote sita walioaga ni wahudumu wa afya wa sadaruki.

kra

Watu wengine 20 wameambukizwa wengi wao wakiwa wahudumu wa afya haswa wale wa sadaruki.

Marburg ni ugonjwa wa unaosababishwa na virusi na dalili zake ni kama vile kuumwa na kichwa ,kutapika,uchovu wa misuli na maumivu ya tumbo .

Serikali inashirikiana na idara mbalimbali kuwatambua waliotangama na aidha wagonjwa au waliofariki kama tahadhari ya kuzuia maambukizi zaidi.

Ugonjwa huo husababisha vifo kwa asilimia 88 ya wagonjwa.

Website | + posts