Home Michezo Simiu Ebenyo ashinda Berlin Half Marathon

Simiu Ebenyo ashinda Berlin Half Marathon

0

Daniel Simiu Ebenyo wa Kenya ndiye mshindi wa makala ya 43 ya mbio za Berlin Half Marathon, zilizoandaliwa Jumapili nchini Ujerumani.

Simiu aliwaongoza wenzake kutamalaki nafasi tano za kwanza akikata utepe kwa dakika 59 an sekunde 30,akifuatwa na Amos Kurgat kwa dakika 59 na sekunde 42, naye Isaia Lasoi akaridhia nafasi ya tatu kwa dakika 59 na sekunde 47.

“Nilikuja hapa Berlin kwa nia ya kuvunja rekodi ya dunia ,ila nilianza kukumbwa na tatizo la goti kuanzia Kilimita 11 na hali ya anga ikawa na joto jingi ,na nikajua siwezi vunja rekodi leo lakini nitajaribu wakati mwingine.”akasema Ebenyo

Mkenya Winnie Kimutai alimaliza wa nne katika mbio za wanawake  zilizoshindwa na  Tekle Muluat wa Ethiopia kwa dakika 66 na sekunde 53.

Website | + posts