Home Michezo Simba yasitisha mkataba na kocha Robertinho

Simba yasitisha mkataba na kocha Robertinho

0

Klabu ya soka ya Simba nchini Tanzania imetangaza kusitishwa kwa mkataba kati yake na mkufunzi mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Gonclaves Do Carmo.

Kwenye taarifa kwa umma, Simba almaarufu wekundu wa msimbazi ilielezea kwamba hilo liliafikiwa baada ya makubaliano ya pande zote.

Mwingine aliyeathiriwa na hali hiyo ni kocha wa viungo Corneille Hategekimana na Simba imeelezea kwamba walikubaliana naye vile vile.

Kocha Daniel Cadena ndiye sasa ametwikwa jukumu la kuifunza timu hiyo ya soka na atasaidiwa na Seleman Matola.

Usimamizi wa klabu ya Simba ulishukuru makocha hao wawili kwa mchango wao na kuwatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya.

Kwenye taarifa hiyo ya leo Novemba 7, 2023, Simba imesema imeanzisha mchakato wa kutafuta makocha wengine kuchukua nafasi za wawili hao, shughuli inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni.