Timu ya taifa ya Cameroon almaarufu The Indomitable Lions imeendeleza mazoezi mjini Yaounde kujiandaa kwa mechi ya tatu ya kundi J, kufuzu kwa fainali za AFCON mwakani dhidi ya Harambee Stars ya Kenya.
Cameroon imepigwa jeki baada ya kurejea kikosini kwa mshambulizi Vincent Aboubakar, Michael Ngadeu Ngandjui, Faï Collins, Christian Bassog, Jackson Tchatchoua na Patrick Soko.
Cameroon na Kenya wanaongoza kundi J kwa alama 4 kutokana na mechi mbili za ufunguzi.
Mchuano huo utasakatwa Ijumaa hii katika uwanja wa Japoma, huku ule wa marudio ukipigwa Jumatatu ijayo Oktoba 14 jijini Kampala Uganda.