Home Kimataifa Siku ya vikosi vya ulinzi KDF kuadhimishwa Jumamosi

Siku ya vikosi vya ulinzi KDF kuadhimishwa Jumamosi

Vikosi vya KDF ambavyo hujumuisha wanajeshi wa angani, wale wa nchi kavu na wanajeshi wa majini. huchukulia siku hii kuwa muhimu sana katika kalenda ya KDF.

0
Vikosi vya Ulinzi KDF.
kra

Sherehe za kuadhimisha siku ya Vikosi vya ulinzi hapa nchini KDF, zitaandaliwa Jumamosi tarehe 14 mwezi Oktoba mwaka huu.

Siku ya KDF huandaliwa kila mwaka, tangu mwaka 2012 wakati ambapo operesheni ya Linda nchi ilipozinduliwa, kukabiliana na wanamgambo wa Alshabab waliozidisha mashambulizi nchini Kenya.

kra

Wakati wa sherehe hizo, wanajeshi ambao wameonyesha utendakazi bora katika majukumu yao, hutuzwa katika kutambua kazi yao ya kupigiwa mfano.

Vikosi vya KDF ambavyo hujumuisha wanajeshi wa angani, wale wa nchi kavu na wanajeshi wa majini. huchukulia siku hii kuwa muhimu sana katika kalenda ya KDF.

Wanajeshi wa KDF, hutekeleza wajibu muhimu wa kuhakikisha amani inadumishwa katika kanda ya Afrika Mashariki.

Vikosi vya KDF ni miongoni mwa vikosi vya muungano wa Afrika ATMIS, vinavyokabiliana na wanamgambo wa Alshabab nchini Somalia.

Pia KDF ni sehemu ya vikosi vya jumuiya ya Afrika Mashariki, vilivyotumwa mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, kukabiliana na wapiganaji wa M23.

Website | + posts