Home Kimataifa Shule zimeagizwa kutekeleza kikamilifu miongozo ya usalama

Shule zimeagizwa kutekeleza kikamilifu miongozo ya usalama

Waziri wa elimu Julius Ogamba alisema wizara ya elimu itaanza ukaguzi wa shule zote za bweni hapa nchini, kuhakikisha miongozo hiyo inatekelezwa.

0
Waziri wa elimu Julius Ogamba.
kra

Wizara ya elimu imetoa agizo kwa shule zote za bweni, kuzingatia kikamilifu miongozo ya usalama iliyopo, ili kuepusha mikasa kama ile iliyotokea katika shule ya Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri.

Katika taarifa, waziri wa elimu Julius Ogamba alisema wizara ya elimu itaanza ukaguzi wa shule zote za bweni hapa nchini, kuhakikisha miongozo hiyo inatekelezwa.

kra

Kulingana na waziri huyo, awamu ya kwanza ya ukaguzi wa huo ulioanza wiki hii, unalenga shule za bweni za msingi na Junior School, huku awamu ya pili ikilenga shule za upili.

Waziri huyo alisema ukaguzi huo utawahusisha maafisa kutoka wizara ya elimu, wale wa usalama wa taifa, maafisa wa afya na vile vile maafisa wa ujenzi.

“Ukaguzi huo utawezesha serikali kubainisha chanzo cha misururu ya moto shuleni iliyoshuhudiwa hivi karibuni, na kutoa mapendekezo mwafaka ya kuzuia visa hivyo,” alisema waziri huyo kupitia kwa taarifa.

Ogamba aliwaonya maafisa wa wizara ya elimu na wasimamizi wa shule, dhidi ya kukiuka miongozo iliyopo ya usalama.

Hatua hiyo ya wizara ya elimu, inajiri siku chache baada ya moto kuteketeza bweni la shule ya Hillside Endarasha na kusababisha vifo vya wanafunzi 21.

Visa vya moto pia vimeripotiwa katika baadhi ya shule kote nchini.

Website | + posts