Home Kimataifa Shule zafunguliwa kwa muhula wa tatu, walimu wa sekondari wasusia kazi

Shule zafunguliwa kwa muhula wa tatu, walimu wa sekondari wasusia kazi

0
kra

Shule za msingi zimefunguliwa kwa muhula wa tatau kote nchini leo Jumatatu huku walimu wa sekondari wakianza mgomo na kushiriki maandamano katika maeneo kadhaa nchini.

Walimu wa shule za msingi wameripoti kazini baada ya chama chao cha KNUT kufutilia mbali mgomo wao jana Jumapili.

kra

KNUT ilikiri kuafikiana na serikali kuhusu utekelezaji wa matakwa yao.

Licha ya kusitisha mgomo, shule nyingi za msingi zimenakili idadi ndogo mno ya walimu walioripoti kazini.

Hata  hivyo, KUPPET imewataka walimu wa shule za sekondari kuendelea kukaa nyumbani hadi serikali itimize matakwa yao.

Mgomo huo huenda ukaathiri pakubwa masomo na mtihani wa kidato cha nne, KCSE unaotarajiwa kuanza  mwezi Oktoba.

Muhula wa tatu pia unatarajiwa kuwa mfupi zaidi ili kupisha mitihani ya kitaifa.

Website | + posts