Home Kimataifa Shule zafunguliwa kwa muhula wa tatu mwaka huu

Shule zafunguliwa kwa muhula wa tatu mwaka huu

0
kra

Shule zinafunguliwa leo Jumatatu Agosti 28, 2023 baada ya likizo ya wiki mbili na wanafunzi wameanza kurejea shuleni.

Kulingana na kalenda ya Wizara ya Elimu, huu ndio muhula wa tatu na wa mwisho mwaka 2023 na utaisha Oktoba 27, 2023.

kra

Huu ndio muhula mfupi zaidi lakini tena muhimu zaidi kwa sababu wanafunzi watafanya mitihani yao ya kitaifa na kwa sababu hizo mbili hakutakuwa na mapumziko ya katikati ya muhula.

Wanafunzi wa taasisi zote za elimu nchini ambao hawako kwenye madarasa ya mitihani ya kitaifa, wataondoka shuleni Oktoba 28, 2023 na watafungua tena Januari 8, 2024.

Wale wa gredi ya 6 na darasa la nane wataanza mitihani yao ya kitaifa ya KPSEA na KCPE Oktoba 30 na kumaliza Novemba 2, 2023.

Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE utaanza Novemba 3 na kukamilika Novemba 24, 2023 huku shughuli ya kusahihisha mitihani hiyo ikianza Novemba 27, 2023.

Kazi hiyo itaendelea kwa majuma matatu hadi Disemba 15, 2023.

Kenya ilirejelea kalenda ya kawaida ya masomo mwaka huu baada ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya korona mwaka 2020.

Website | + posts