Shule ya upili ya wasichana ya Kisumu imefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia mgomo wa wanafunzi.
Inasemekana kwamba wanafunzi walitaka burudani shuleni humo jana usiku na usimamizi ulipokosa kuridhia wakagoma.
Wanafunzi hao walipiga kelele usiku kucha shuleni humo wengine wakiamua kukesha kwenye uwanja wa shule.
Usimamizi wa shule hiyo umeamua kuruhusu wanafunzi kuondoka shuleni humo na kukaa nyumbani kwa muda usiojulikana kama njia ya kutuliza hali.