Home Habari Kuu Shule kadhaa zawarejesha wanafunzi nyumbani

Shule kadhaa zawarejesha wanafunzi nyumbani

Kangemi na Kibra ni baadhi ya mitaa kaunti ya Nairobi, ambayo imekumbwa na visa vingi vya maandamano na uharibifu wa mali .

0

Shule kadhaa katika mitaa ya kaunti ya Nairobi zimewarejesha wanafunzi nyumbani licha ya agizo la serikali la jana Jumatano kuzitaka shule zote za kutwa kaunti za Nairobi, Mombasa na Kisumu kufunguliwa leo.

Shula kadhaa za mitaa ya Kibra na Kangemi ziliripotiwa kuwataka wanafunzi waliofika shuleni kwa masomo kurejea nyumbani kwa kuhofia usalama wao.

Baadhi ya shule ziliwataka wanafunzi kurejea shuleni kesho Ijumaa, yamkini lengo likiwa kutathmini hali ya usalama zenyewe hata baada ya serikali kuwataka wanafunzi kurejea shuleni.

Maandamano ya upinzani dhidi ya serikali yaliyoanza jana Jumatano yanaingia siku ya pili leo Alhamisi.

Kangemi na Kibra ni baadhi ya mitaa kaunti ya Nairobi, ambayo imekumbwa na visa vingi vya maandamano na uharibifu wa mali.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here