Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande maarufu kama
Shujaa,imefuzu kwa fainali ya kurejea kwa mashindano ya msururu wa dunia HSBC.
Kenya ilimaliza ya pili katika mashindano ya mchujo yaliyoandaliwa mjini Munich Ujerumani mwishoni mwa juma lililopita, na kujikatia tiketi kwa fainali itakayoandaliwa Madrid Uhispania.
Shujaa walipoteza pointi 19-17 dhidi ya Ujerumani katika robo fainali na kisha kuinyuka Uganda alama 48-0 na kumaliza katika nafasi ya tano.
Kenya itajiunga na tomu za Uruguay walioshinda mchujo wa Munich,Ujerimani na Chile pamoja na timu nyingine nne zilizoshushwa ngazi kutoka kwa mashindano ya msururu wa dunia.
Timu hizo nane zitatengwa katika makundi mawili huku mshindi wa jumla, akifuzu kushiriki mashindano ya msururu wa dunia mwaka ujao.