Home Kimataifa Shujaa walamba sakafu Olimpiki baada ya kucharazwa na Samoa

Shujaa walamba sakafu Olimpiki baada ya kucharazwa na Samoa

0
kra

Timu ya taifa ya Raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande imepoteza fursa ya kutwaa medali katika michezo ya Olimpiki inayoendelea jijini Paris Ufaransa, baada ya kupigwa laza alama 26-0 katika mechi ya mwisho ya kundi B Alhamisi jioni.

Samoa walichukua uongozi kupitia kwa try ya kipindi cha kwanza iliyofungwa na Matou Opetai’s .

kra

Paul Scanlan, Vaa Maliko na Steve Onosai waliongeza try moja kila moja, huku Faafoi Falaniko, Tom Maiva na Neueli Leifufia wakiongeza conversion moja kila mmoja.

Kipigo hicho pia kilizima ndoto ya Kenya kusajili matokeo bora kuliko yale ya Tokyo Japan miaka mitatu iliyopita, walikomaliza katika nafasi ya 9.

Timu hiyo inayofunzwa na kocha Kevin Wambua itakabiliana na Uruguay baadaye leo usiku kwa mchuano wa kuwania nafasi ya 9 ahdi 12.

Katika mechi za kwota fainali Afrika Kusini itapambana na New Zealand nao Argentina wamenyane na wenyeji Ufaransa.

Mabingwa watetezi Fiji watakabana koo na Ireland huku Australia ikikamilisha ratiba dhidi ya Marekani Alhamsi usiku.