Home Kimataifa Shughuli za uokoaji zaendelea Kiamaiko ambako jengo liliporomoka

Shughuli za uokoaji zaendelea Kiamaiko ambako jengo liliporomoka

0
kra

Shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo la Kiamaiko katika kaunti ya Nairobi ambako jengo liliporomoka.

Kulingana na shirika la msalana mwekundu nchini, watu wanne wameokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo ambalo lilikuwa linabomolewa katika eneo la Mathare North Area 1.

kra

Shirika hilo kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook limeelezea kwamba mipango inaendelea ya kufikia na kuokoa watu wengine ambao wanaaminika kufunikwa na vifusi hivyo.

Watatu kati ya waliookolewa walipelekwa kwa hospitali iliyo karibu kwa ajili ya matibabu huku mmoja aliyekuwa na majeraha madogo akitibiwa katika eneo la mkasa.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya jengo la orofa tano kuporomoka kwenye barabara ya Naivasha huko Uthiru jijini Nairobi lakini kwa bahati nzuri hakuna maafa yaliyoripotiwa.

Nyumba zilizojengwa mahali pasipostahiki na zilizo karibu na mito zimekuwa zikibomolewa na serikali kama njia moja ya kuhakikisha usalama wa raia hasa baada ya kero la mafuriko.