Home Burudani Shughuli ya kupiga kura kwa tuzo za TMA yaendelea

Shughuli ya kupiga kura kwa tuzo za TMA yaendelea

0
kra

Wapenzi wa muziki nchini Tanzania wana fursa ya kuwapigia kura wanamuziki wawapendao kwenye tuzo za TMA yaani Tanzania Music Awards.

Kipindi cha kupiga kura kilifunguliwa rasmi Septemba 3, 2024 baada ya orodha ya wawaniaji wa tuzo kwenye vitengo 17 kutangazwa rasmi na waandalizi.

kra

Siku ya mwisho ya kupiga kura ni Septemba 28 huku siku ya kutoa tuzo hizo ikiwa Septemba 29, 2024.

Wanamuziki tajika nchini Tanzania Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize wameteuliwa kuwania tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, huku Zuchu, Nandy, Anjella na Malkia Leyla Rashid wakiwa kwenye kitengo sawia upande wa kina dada.

Talanta zinazoibukia katika ulingo wa muziki nchini humo pia hazijasaazwa ndiposa kitengo cha mwanamuziki mpya wa mwaka kikabuniwa ambapo Appy, Xouh, Chino Kidd, Yammi na Mocco Genius watapambana.

Kamati andaizi ya tuzo hizo ikiongozwa na mwenyekiti David Minja na naibu mwenyekiti Christine Seven Mosha ilitangaza kwamba kampuni ya Pepsi ndiyo mdhamini mkuu wa tuzo hizo mwaka huu.

Katika upeperushaji wa moja kwa moja wa hafla ya kutoa tuzo, Mosha katika mkutano na wanahabari alisema kwamba wameshirikiana na MTV Africa na BET.

Awali wasanii walilalamikia jinsi tuzo hizo huandaliwa na jinsi washindi huteuliwa na mwaka huu wadadisi wako ange kuona mambo yatakavyokuwa.

Website | + posts