Home Habari Kuu Shirikisho la mpira wa kikapu Marekani kukuza talanta mashinani

Shirikisho la mpira wa kikapu Marekani kukuza talanta mashinani

0

Shirikisho la mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani National Basketball Association -NBA limejitolea kutekeleza mipango ya kukuza talanta za mchezo huo mashinani nchini Kenya.

Haya yalibainika wakati maafisa wa shirikisho hilo la NBA walimzuru Rais William Ruto katika ikulu ya Nairobi.

Waliokuwepo ni pamoja na mkurugenzi mtendaji wa NBA Victor Williams, bingwa mara tano wa NBA Ron Harper na aliyekuwa mchezaji wa NBA Micheal Finley.

Waliandamana na balozi wa Marekani nchini Meg Whitman na waziri wa michezo Ababu Namwamba.

Rais Ruto alisema kujihusisha na michezo kitaalamu kunaweza kubadilisha maisha ya vijana wengi humu nchini.

Mipango ya NBA nchini ya kukuza na kuimarisha talanta itaanza mafunzo kwa wavulana na wasichana 70 na kufunguliwa kwa afisi ya 5 ya NBA barani Afrika jijini Nairobi.

Haya yaliafikiwa kupitia mkataba ambao ulitiwa saini na shirikisho la NBA Septemba 2023 jijini New York nchini Marekani.

Wawakilishi hao wa NBA walimkabidhi Rais Ruto sare ya timu ya Lakers na mpira.

Website | + posts