Home Habari Kuu Shirika la reli nchini lasimamisha utoaji huduma kutokana na mafuriko

Shirika la reli nchini lasimamisha utoaji huduma kutokana na mafuriko

Kupitia kwa taarifa Jumatano asubuhi, usimamizi wa shirika hilo ulisema  hatua hiyo ilichukuliwa kuhakikisha usalama wa wasafiri.

0
Huduma za uchukuzi wa gari moshi wasimamishwa.

Shirika la reli nchini, limesitisha utoaji wa huduma, kutokana na mvua kubwa inayonyesha hapa nchini, baada ya reli kuathiriwa na mafuriko.

Kupitia kwa taarifa Jumatano asubuhi, usimamizi wa shirika hilo ulisema  hatua hiyo ilichukuliwa kuhakikisha usalama wa wasafiri.

“Tunafahamisha umma kuwa uchukuzi kupitia gari moshi umesimamishwa kwa muda kutokana na mvua kubwa inayoshuhudiwa ambayo imeathiri reli. Tumelazimika kuchukua hatua hiyo kwa sababu usalama wa wateja wetu ni jukumu letu,” ilisema taarifa hiyo.

Hata hivyo shirika hilo limesema litatangaza kurejelewa kwa huduma zake.

“Tutawashauri punde tu huduma za kawaida zitakaporejea. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na hatua hiyo,” iliongeza taarifa hiyo.

Website | + posts