Home Habari Kuu Shirika la IMF laidhinisha mkopo kwa Kenya

Shirika la IMF laidhinisha mkopo kwa Kenya

0

Shirika la hazina ya kimataifa ya fedha IMF limeidhinisha mkopo mwingine kwa serikali ya Kenya, baada ya kutimiza mahitaji yote kwenye awamu ya tano ya uhakiki. Mkopo huo wa shilingi bilioni 142, uliidhinishwa Jumatatu, Julai, 17, 2023.

Awali shirika la utafiti la EFG Hermes Research lilikuwa limesema kwamba Kenya ilikuwa inahitaji sana mkopo huo kutoka kwa IMF kusaidia kuhifadhi hazina zake za nje wakati ambapo dhamana yake ya bilioni 283 almaarufu Eurobond inatizamiwa kukomaa Juni, 2024.

Pesa hizo ambazo Kenya imepata kutoka kwa IMF zitatumika kupunguza uhaba wa pesa kwenye hazina kuu nchini na kusaidia kukuza mageuzi katika uchumi na tabia nchi.

Kulingana na IMF, shilingi bilioni 56 zitaelekezwa katika kuongeza akiba ya Kenya ya pesa za kigeni na kukuza uchumi. Hizo pesa zingine za juu zilitolewa chini ya mpango wa IMF wa kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Haya yanajiri wakati ambapo shilingi ya Kenya inaendelea kushinikizwa katika soko la ubadilishanaji wa fedha huku mpango wa serikali hadi serikali wa mafuta uliokuwa ukilenga kunusuru shilingi ya Kenya ukikosa kuafikia mengi.

Uchumi wa Kenya umestahimili sana hata baada ya taifa kukubwa na kiangazi kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi na mazingira mabaya ughaibuni.

Jumapili rais William Ruto alionyesha kuridhika kwake kuhusu hatua ya bara hili kupokea fedha zaidi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here