Home Michezo Shabana FC wailewesha Tusker wakisajili ushindi wa kwanza ligini

Shabana FC wailewesha Tusker wakisajili ushindi wa kwanza ligini

0

Shabana FC imeandikisha ushindi wa kwanza katika ligi kuu FKF, baada ya kuwalemea Tusker FC bao moja kwa bila mchuano uliosakatwa Ijumaa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Shabana ambao hawakuwa wameshinda mechi yoyote katika michuano mitano ya ufunguzi, walihitaji bao la dakika ya 70 kupitia kwa bao lililofungwa kwa kichwa na Vincent Nyabuto,akiunganisha mkwaju wa adhabu wa Rodgers Aloro.

Kwenye matokeo mengine ya Ijuma Kakamega Homeboyz walilazimishwa kutoka sare ya 3-3 na Talanta FC huku viongozi wa ligi Posta Rangers wakiibwaga Nzoia Sugar magoli mawili kwa nunge.

Shabana wamechupa hadi nafasi ya 14 katika jedwali kwa alama 6 kufuatia michuano 6 wakipiga sare tatu na kupoteza mara mbili na kunakili ushindi mmoja.

Website | + posts