Home Michezo Shabana FC na Murang’a Seal zaingia ligi Kuu FKF

Shabana FC na Murang’a Seal zaingia ligi Kuu FKF

Baada ya mechi 34 za ligi hiyo Shabana na Muranga zina idadi sawa ya pointi 64 ingawa Shabana wangali na mechi moja mkobani.

0

Shabana FC yenye makao yake katika kaunti ya Kisii na Muranga Seal zilifuzu kucheza ligi kuu ya FKF msimu ujao, kufuatia ushindi wa wa mechi za Juampilj katika ligi kuu ya kitaifa ya Super (NSL).

Shabana waliishinda Migori Youth ugenini bao moja kwa bila huku Muranga Seal pia wakipata usbindi uo huo ugenini kwa Coastal Heroes.

Baada ya mechi 34 za ligi hiyo Shabana na Muranga zina idadi sawa ya pointi 64, ingawa Shabana wangali na mechi moja mkobani.

Shabana ambayo ni timu ya tatu kwa ufuasi mkubwa baada ya Gor Mahia na AFC Leopards katika historia ya Kenya ,walishiriki ligi kuu ya Kenya kwa mara ya mwisho mwaka 2006 ,ilihali Muranga wanajiunga na ligi kuu kwa mara ya kwanza.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here