Home Habari Kuu Serikali za kaunti zalaumiwa kwa utumizi mbaya wa fedha

Serikali za kaunti zalaumiwa kwa utumizi mbaya wa fedha

Alitambua mianya iliyopo katika mbinu za kujipatia mapato,huku akitoa changamoto kwa utawala wa kaunti kuimarisha mifumo yao ya kukusanya mapato.

0
Msimamizi wa bajeti, Margeret Nyakango.

Msimamizi wa bajeti, Margeret Nyakango amezikosoa serikali za kaunti kwa matumizi mabaya ya rasilimali za umma,hususan kwa shughuli za usafiri na utalii badala ya maendeleo.

Wakati wa ziara ya uangaziaji na utathmini katika kaunti ya Busia, Nyakango aligusia ukosefu wa vifaa vinavyohitajika katika kaunti nyingi, ikiwemo Busia katika utekelezaji wa miradi kwa kuangazia utalii badala ya maendeleo.

Alitambua mianya iliyopo katika mbinu za kujipatia mapato,huku akitoa changamoto kwa utawala wa kaunti kuimarisha mifumo yao ya kukusanya mapato.

Naibu gavana wa kaunti ya Busia Arthur Odera, alipongeza juhudi zilizoimarishwa na kaunti ya Busia katika mbinu za utekelezaji ambapo alielezea kujitolea kwa serikali za kaunti kushirikiana na msimamizi wa bajeti ili kuhakikisha ugatuzi unafaulu.

Website | + posts