Home Kaunti Serikali yazindua mradi wa maji wa shilingi million 90 West Pokot

Serikali yazindua mradi wa maji wa shilingi million 90 West Pokot

0

Wakaazi wa baadhi ya maeneo ya kaunti ya Pokot Magharibi kama Chepareria, Kipkomo, Senetwa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuzindua mradi wa maji wa kima cha shilingi million 90.

Akizindua mradi huo, katibu wa maji na usafi Julius Korir alisema kuwa zaidi ya nyumba 50,000 zitanufaika.

Vile vile, aliweka jiwe la msingi kwa mradi mwingine katika tarafa ya Mtembur-Kitalakapel utakaofaidi nyumba 11,000.

Katika zoezi hili, Korir alisema, “kupatikana kwa maji ya kutegemewa ni muhimu kwa afya ya umma,elimu na ukuaji wa uchumi, jambo ambalo linafanya mradi huu kuwa uwekezaji muhimu kwa maendeleo ya jamii hii.”

Katibu huyo alikuwa ameandamana na gavana wa kaunti hiyo Simon Kachapin, mbunge wa Kapenguria Samuel Moroto na naibu kamishna Wycliffe Munanda.