Home Kaunti Serikali yazindua huduma za mtandao kwenye kaunti ndogo

Serikali yazindua huduma za mtandao kwenye kaunti ndogo

Wizara ya habari,mawasiliano na uchumi wa kidijitali kwa ushirikiano na serikali ya Ubelgiji, imezindua huduma za mtandao kwenye kaunti ndogo humu nchini.

Kupitia mradi wa kuunganisha maeneo hayo kwenye mtandao,mitambo 753 ya kutoa huduma hizo imewekwa kwenye kaunti 46 hapa nchini, huku serikali ikifanya juhudi za kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapatikana katika maeneo ya mashinani.

Akiongea wakati wa mkutano wa wadau katika kaunti ya Kisumu, mkurugenzi wa usimamizi kwenye wizara ya habari Jeremiah Munayi, alisema miradi hiyo inalenga afisi muhimu za umma katika juhudi za kuimarisha mawasiliano  na pia kuwezesha wananchi  kupata huduma kupitia mtandao.

Alisema  kwamba serikali imeongeza huduma zinazotolewa kupitia mtandao ili kuwawezesha wakenya mashinani kupata huduma hizo.

Munayi alisema mradi huo pia unalenga kuunga mkono mpango wa kiuchumi wa serikali wa Bottom-Up huku mamilioni ya wakenya wakiweza kupata huduma hizo za mtandao na hata kufanya biashara zao kupitia huduma hizo.

Kwa upande wake kamishna wa kauntui ya kisumu Hussein Alassow Hussein, alisema mradi huo ni nguzo muhimu katika kuimarisha mawasiliano ndani ya serikali.

Alidokeza kuwa serikali imewekeza mabilioni ya pesa kuweka miundo msingi, huku akitoa wito kwa idara za serikali za kaunti na kitaifa kutumia kikamilifu rasilimali hiyo.

Website | + posts
Radio Taifa
+ posts